Anzia ulicho nacho, anza kidogo na uzishinde changamoto ukitumia maarifa zako.

Submitted by admin on Fri, 02/13/2015 - 00:00
Display title
Anzia ulicho nacho, anza kidogo na uzishinde changamoto ukitumia maarifa zako.
Bio
Image
Display name
Rusia Orikiriza – Uganda
Orikiriza Rusia Bariho alianzisha Oribags Innovations Ltd, iliyoko Kampla, Uganda mnamo mwaka wa 2009. Biashara kuu ya Oribags Innovations ni kuruwaza, kutengeneza na kuuza mifuko isiyodhuru mazingira inayotengenezwa na takataka za ukulima, taka za makaratasi na taka za unyuzi halisi.


Story

Safari yangu kama mjasiriamali mwanamke haijakuwa rahisi. Hii ni kwa sababu nafasi haziwajii kwa urahisi majasiriamali nchini Uganda, haswa wanawake.

Nilizaliwa na kulelewa katika kijiji kidogo cha Kabale, kusini magharibi wa Uganda. Nilipokuwa mdogo sana, mamangu alinifunza kufuma vikapu na kutengeneza shanga pamoja na mapambo ya vito huku babangu akifanya kazi ya ukulima wa mananazi.

Wazazi wangu wamekuwa misukumo mikuu kwangu. Mamangu alinifuza mbinu zangu za ujasiriamali na misingi ya biashara. Nilifanya kazi naye katika biashara yake nikitengeneza pombe la kienyeji liitwalo ‘tonto’ ambayo aliuzia baa za mitaani. Kupitia biashara yake, alichanga pesa za kulipa karo zetu na kuyakidhi mahitaji mengine ya familia.

Familia yetu haingeweza kugharamia elimu yangu ya shule ya upili lakini jamaa alijitolea kunisaidia ili niweze kuendeleza elimu yangu. Hili tendo la ukarimu lilinitia moyo na kunifunza mambo mengi yakwemo manufaa ya adabu na uwajibikaji wa mtu kwa familia yake na jamii kwa jumla. Sikufahamu wakati huo kwamba hii heshima kwa hadhi ya utu baadaye ungekuja kuwa ushawishi muhimu katika maisha yangu binafsi na kuielekeza mbinu yangu ya kuongoza na kuwafunza wafanyikazi.

Katika elimu yangu yote, nilijua kwamba njia pekee ya kutamatisha mukwamo wa umaskini ilikuwa ni kufanya bidii, na kuanza kupata pesa mapema iwezekanavyo. Hivyo basi, baada ya masomo yangu ya sekondari, nilianza kuuza mitumba kupitia akiba zangu. Pia, nilijotolea kama mratibu wa vijana katika African Medical Research Foundation wakati wa likizo zangu.

Baada ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere, nilianza kutengeneza kwa mikono na kuuza mapambo ya vito kwa kutumia mbinu nilizofunzwa na mamangu. Niliyatengeneza mapambo hayo ya vito kutoka kwa taka za makaratasi nilizotoa kwa ofisi za chuo. Nilipata hela za kutosha kunisitiri na pia za kuwasaidia wazazi wangu kulipa karo za ndugu zangu.

Katika mwaka wa 2007, serikali ya Uganda ilipiga marufuku uingizaji nchini kutoka ng’ambo, uuzaji na utengenezaji wa mifuko ya plastiki. Watu wengi hawakuwa na njia mbadala kwa mifuko ya plastiki.

Niligundua kwamba taka za makaratasi nilizokuwa nikitumia kutengeneza mapambo ya vito zingeweza kugeuzwa mifuko ya karatasi.

Kwa hivyo, katika mwaka wa 2009, nilianzisha kampuni yangu, Oribags Innovations na dola mia 300 za marekani nilizozitengeneza kutoka kwa biashara yangu ya mapambo ya vito.

Kuifanya kampuni yangu ya Oribags Innovations kukua haijakuwa rahisi. Imekuwa matokeo ya msimamo wangu mkali na kujitolea kwangu. Kwa zaidi ya miaka miwili, nilitenda kazi bila faida na nilijitahidi kuidumisha biashara. Hata hivyo, nimewahi pata usaidizi mwingi njiani. Mlezi wangu na marafiki zangu wamenipa usaidizi na mawaidha chungu nzima. Nilipowasilisha wazo langu la kibiashara kwa Uganda Industrial Research Institute (UIRU), walinipa nafasi ya kuifanyia kazi. Watafiti wa UIRI vilevile walinisaidia kupata mbinu mwafaka wa kutumia tena vifaa tuanavyo mashinani kama vile maganda ya mgomba, na nguo/vitambaa za zamani.

Oribags kwa sasa imewapa kazi watu 19 wakiwemo wanawake 13 na wanaume sita. Ndoto yangu kwa Oribags ni kuifanya mzalishaji mkuu wa bidhaa na huduma zisizodhuru mazingira katika maeneo ya Afrika Mashariki ifikapo mwaka wa 2020. Nina fuhara kwamba Oribags tiyari ipo katika mkondo wa kuifikia uwezekano huu.

Wafanyikazi wangu pamoja nami hutengeneza mifuko kwa kutumia mikono yetu yenye kipaji, mmoja baada ya mwingine, kupitia teknolojia ya rahisi yenye mtindo usiotoa kaboni yoyote na na unaosistiza urembo asilia dhidi ya ukamilifu wa kimashine. Tumetengeneza mbinu ya mtungo wa thamani kwa kuwatia motisha wakulima na wengine wanaotupa malighafi. Sekta ya kimataifa ya mifuko ya makaratsi inapoendelea kutumia karatasi zinazotoka mitini, Oribags Innovations hutengeneza mifuko yake kutokana na malighafi za kitamaduni kama vile maganda ya migomba na mabaki ya pamba.

Katika safari hii yote, nimejifunza mengi. Ili kuanzisha biashara, anzia ulicho nacho. Nimekuja kutambua kwamba ushauri na mifumo ya mitandao ni muhimu, na kwamba ni afadhali kuanza kwa kiwango kidogo. Mbinu unazozikuza unaposhinda changamoto za kustawisha biashara yako zina thamani kubwa kupindukia.

Ninagundua kwamba wnawake wengine bado wanadharau aina fulani za kazi. Wanasahau kwamba idadi kubwa ya biashara za kimataifa zenye fanaka zilianza kwa kiwango kidogo tu. Tukibadilisha fikira zetu, basi killa manamke atawezeshwa kote ulimwenguni. Kuna kiasi kikubwa cha nafasi za kiasii zinazotuzunguka na katika jamii zetu zinazoweza kubadilisha maisha yetu. 

Maswali kwa msomaji:

1. Ni hadhi na mbinu za kibinafsi za aina gani unazozileta kutoka utotoni mwako na matukio ya maisha yako yanayoweza kujenga au kuimarisha biashara yako?

2. Je, waona changamoto kama hizi katika nchi yako ambazo ungetatua kwa njia ya biashara? Kumbuka kwamba nafasi kila mara zinawezajificha katika shida.

3. Je, ndoto yako ya kudumu ya nia zako, suluhisho na biashara ni zipi?

Lessons
1. Uchanganuzi wa soko: kuna mahitaji na nafasi katika jamii yako unazoweza kuzitatua kwa kutumia mbinu zako za kibinafsi za biashara. 
 

2. Ukuaji wa biashara: anzia ulicho nacho, jifunze kupitia makosa na changamoto unazokumabana nazo njiani, na uangazie yanachokufanya ufaulu. 

3. Kutengeneza mitandao: tafuta na ukubali usaidizi kutoka kwa watu wenye ujuzi na vipawa na wanaoweza kukutia motisha kupitia mawazo mapya na kukusaidia kukuza biashara yako.