Changanya utamaduni, desturi, na uvumbuzi katika mfumo wa biashara yako.

Submitted by admin on
Display title
Changanya utamaduni, desturi, na uvumbuzi katika mfumo wa biashara yako.
Bio
Image
Display name
Asmaa Benachir – Morocco
Asmaa Benachir – alipata mmafunzo kama msanii wa sanaa za kutazamwa kabla ya kuwa mojawapo wa waanzilishi na rais wa Shirika la Moroccan Signatures la kuendeleza na kudumisha Sanaa na utamaduni nchini Morocco. Alianzisha Au Grain de Sesame mnamo Desemba mwaka wa 2007 katika Rabat Medina, iliyoshinda tuzo la UN SEED award katika mwaka wa 2013.


Story

Katika miaka ya 1990, nilikuwa mmoja wa waanzilishi wa Moroccan Signatures, shirika wa kuendeleza usanii na utamaduni nchini Morocco. Kufikia mwaka wa 2007, niliwahi hudumu kama Rais kwa miaka kumi na hii tajriba ilinihakikishia kwamba usanii huwawezesha watu kutoka jamii ndogondogo kuishi maisha mazuri. Hivyo basi, niliacha wadhifa wangu na kutumia siku za maisha yangu kuianzisha Au Grain de Sésame (Sesame Seed).

Ninaamini kwamba watu ni kama mbegu dogo. Kila mmoja ana uwezo wa kuwa kitu kikubwa kumshinda. Katika Ali Baba na Wezi 40, Sesame Seed ilikuwa na uwezo wa kufungua milango. Huu mbegu dogo unavyokua, inatupa uwezo wa kuvunja vizuizi na kufikia viwango vipya yva maarifa na maelewano baina ya tamaduni mbalimbali.

Katika mwaka wa 2009, kwa hisani ya usaidizi wa kifedha kutoka kwa rafiki na mshiriki wa kibiashara, niliweza kuzindua literacy café Au Grain Sesame.

Habari kuhusu kuzinduliwa zilienea haraka kupitia vyombo vya habari na baada ya mazungumzo kadhaa na wanawake wa mitaani juu ya mahitaji na azimio zao za kuimarisha maisha yao, niliamua kushiriki nao maarifa na tajriba zangu kama msanii mbunifu na msanii mchoraji nchini Morocco. 

Wengi wa wanawake hawa ni wafanyikazi wa ufundi lakini tofauti na wasanii wanaume wa mitaani, wao hawajasoma na hawajui jinsi ya kutafuta soko na kuuza bidhaa zao kimamilifu. Wanawake wengi wa mitaani ambao wanaobobea katika ushonaji wanaweza tengeneza mshono wowote au ruwaza wanaofunzwa lakini hawawezi kutengeneza nakshi zao. 

Nimekuwa nikifanya majaribio na innovative technique katika kutumia recycled karatasi kutengeneza bidhaa za ecological zikwemo artistic packaging, samani na mapambo za kutani. Mamo Desemba 2010, nianza kufanya warsha kuwafunza wanawake wasiobahatika kule Rabat/Salé Medina sanaa na vifaa vya sanaa ya mkono visivyoghali.

Wanawake waliohudhurua warsha hiyo walijifunza mbinu mpya za kurembesha zinazochanganya mbinu za usanii za kikwetu za kutumia tena vifaa vya kiasilia.

Pia, wanapata mafunzo katika maendeleo ya kisanii na maendeleo ya kibinafsi ju ya wanalowezafanya kuhifadhi urithi wa kitamaduni na mazingira na pia wanajifunza juu ya haki za kijamii na zile za leba.

Baada ya hii, wanawezapata pia elimu endelezi kuhusu jinsi ya kufanya kazi nyumabani, kuanzisha biashara ndogo, au kuanza shirika. Zaidi ya wanawake 50 tayari wamenufaika kutokana na haya mafunzo mafupi.

Chumba chetu cha maonyesho ya warsha ndiyo pato kuu la kituo hiki. Mwanzoni, kutumia kiasi kidogo cha pesa ya uwekezaji tulichokuwa nacho, tulitengeneza mkusanyiko mdogo wa bidhaa. Bidhaa zetu za kipee ziliwavuta wateja wa aina mbalimbali, wa kinyumbani na kimataifa. Tulianza kuweka matawi na kujaribu bidhaa na mbinu mpya na hata tukatengeneza vipande kwa asilimia ya faida juu ya bei zao. Kuchanganya pamoja mbinu kutoka kazi za kitamaduni za mikono na mbinu za practices za kisasa zaidi na za kimataifa zinatuwezesha kudumisha urithi wa utamaduni wetu huuku tukikuza pia njia mpya za sura ya kiusanii.

Takataka za makaratasi nchini Morocco ni shida kuu haswa wakati wa mitaani na uchaguzi wa kitaifa ambapo makaratasi hutawanywa katika barabara na maduka ya kupiga chapa hufanya kazi usiku na mchana kutengeneza vifaa vya kampeni vinavyoishia kuwa taka. Au Grain de Sésame huzitumia tena makaratasi na huzitumia kama kifaa kikuu kutengeneza bidhaa zake zote.

Kituo chetu huendeshwa na wanawake watatu na mwanamume mmoja na kimefaulu kiasi kwamba sasa kimehama majengo yake ya kwanza hadi kwa jumba la kitamaduni inayopakana na yale majengo ya awali. Lakini bado kipo katikati mwa jiji kongwe, kituo cha urithi cha kimataifa cha UNESCO. Majengo hayo yanasetiri chumba cha fani na mchoro mkahawa wa kujifunza kusoma na kuandika, na chumba cha maonyesho. Majumba ya zamani yanakarabatiwa huku karakana mpya za kituo hiki kwa usaidizi wa kifedha kutoka kwa SEED Initiative na pia imefadhiliwa kifedha kiasi na United Nations Environment Programme. 

Wakati huo huo, tunaifanyia kazi mradi wa kupunguza idadi ya miti inayotumika kutengeneza makaratasi. Kwa kulinganishwa na makaratasi taka zisizoweza kutumika tena, makaratasi taka zinazotumika tena hutumia nishati kati ya mara mbili au tatu kidogo zaidi na hutoa kaboni chini ya 30%.

Maswali kwa msomaji:

  1. Ni ujuzi wa kitamaduni na utamaduni zipi katika jamii yako ambazo ungeweza kujengea misingi ili kutengeneza nafasi za kazi?
  2. Wawezaje kuchangia maendeleo ya kudumu kwa kutumia tena na tena vifaa za biashara yako?
Lessons
  1. Mielekeo ya soko: masoko hutafuta ubunifu kila mara na bidhaa za uvumbuzi ambazo ni za kipekee. Tumia aina za sura mbalimbali za kitamaduni katika jamii yako kutengeneza mawazo ya kipekee ya biashara.
  2. Wafanyikazi: imarisha hadhi ya ujuzi na maarifa ya kitamaduni za jamii yako kupitia mafunzo ya ujuzi halisi na kwa kufanya kisasa uzalishaji ili kutengeneza bidhaa yenye soko nchini, kitaifa na kimataifa.