Kukuza biashara kunahitaji bidhaa ya kipekee na yenye sifa nzuri.

Submitted by admin on
Display title
Kukuza biashara kunahitaji bidhaa ya kipekee na yenye sifa nzuri.


Story

Kuendesha biashara sio kitu unachojifunza ghafla. Haswa kwa wanawake wanaoishi mashambani, kuanzisha na kukuza kampuni sio kazi rahisi. Nadharia za kibiashara zinaweza kukusaidia lakini la muhimu zaidi ni kwamba utendaji tu ndio hudhoofisha ukosefu wa uzoefu. 

Katika mwaka wa 2011 tulipoanzisha muungano wetu unaoitwa Latza Velooa – Llano de Mariposa Sociedad de Production Rural Ltd, tulikuwa wanachama wanawake 30 ambao walitumai kujijengea mapato kupitia utengenezaji na uuzaji wa matunda ya mikebe. Makao yetu makuu ni baraza la mji wa Santa Maria Yavesía, iliyoko katika jimbo la kaskazini la eneo la Oaxaca Sierra la Mexico.

Pengine kwa sababu ya ukosefu wetu wa uzoefu, wanachama wengi walijiondoa katika muungano wetu katika hatua za mwanzoni. Ni wanachama wanane tu kati ya wanachama waanzilishi ndio waliobaki. Hata hivyo, tuliamua kuendelea kufanya kazi pamoja tukitumia mafundisho ambayo tulikuwa tumejifunza hadi hatua hiyo. Tulianza polepole huku tukiliimarisha kampuni letu na kujaribu kufanya maamuzi mazuri zaidi. Hata hivyo, tulikuwa tayari kujaribu na pia tulijikaza kutoogopa kufanya makosa kwa vile tulifahamu kwamba kutofaulu kwetu pia kungetufunza mafunzo muhimu sana.

Ukosefu wa rasilmali ulikuwa changamoto yetu ya pili. Tulianza utengenezaji wa siagi yetu ya kwanza kwa kutumia mavuno ya stroberi, tufaha na pichi. Lakini mauzo hayakuwa mazuri jinsi tulivyotarajia na hatukutengeneza faida ambayo ingetuwezesha kukua na kuimarika. Tulikaa chini na kuchanganua jinsi tungeweza kuimarika. Jambo la kwanza tulilofanya ni kusistiza ubora wa bidhaa yetu.

Hatimaye, tulitengeneza upya michakato yetu kwa minajili ya mahitaji ya soko huku tukiunda vibandiko vilivyo na majedwali ya lishe, alama bainifu ya kampuni na nambari ya siri ya kila bidhaa.

Kulisimamia kampuni kumekuwa na changamoto lakini yenye mafunzo tele. Kwa mfano, mwanzoni tuligawana faida baada ya kila miezi sita. Siku hizi, tunajilipa mishahara kila mwezi na hii inatuwezesha kuwekeza katika biashara yetu wenyewe na kwa hakika tumeona manufaa ya kuwa na biashara na kutujitengenezea mapato yetu. Katika nyakati zenye wateja wengi, kampuni huwaajiri wanawake wengine mjini na hii husaidia katika ukuaji na uendelezaji wa mji. Hii ni muhimu kwa sababu hutusaidia kuuchangamsha mji wetu kila mara kwani watu wengi wamehamia Marekani kwa sababu ya ukosefu wa kazi hapa nyumbani.

Lengo la muda mfupi la Latza-Velooa ni kuawaajiri wanawake zaidi kutoka mjini na kujaza malighafi zinazozalishwa na jamii yenyewe. Tuko na uhakika kwamba kupitia usaidizi wa wanachama wetu, kazi yetu, juhudi na pia kwa nehema za Mungu, tutaweza.

Kama wajasiriamali wanawake, tumejifunza vitu vingi. Sasa tunafahamu kwamba kufanya kazi pamoja katika njia ya kukubaliana inatuwezesha kufanya mengi kuliko tukifanya kazi kibinafsi. Pia, tumejifunza kwamba ukitaka kusonga mbele, hakuna vizuizi. Hakuna mpaka wa umri, mahitaji ya kielimu, na pia matatizo ya kuwa mwanamke. Tunayo mahitaji ya kimsingi ya elimu tu na umri wa wanachama wetu, wakiwa wanawake wote na ni kati ya 20 na 65.

Mwakilishi wetu, ijapokuwa ndiye mmoja wa wale walio na umri mdogo sana katika kampuni letu, hutuonyesha kila mara jinsi kazi na kushikilia msimamo thabiti ni mambo muhimu ya kuvuka vizuizi na kusonga mbele. 

Kwa hivyo, jinsi tulivyosema hapo mwanzoni, tumekuja kuamini kwamba ijapokuwa kuanzisha biashara kunahitaji kiasi fulani ya nadharia, biashara inayofaulu hutokana na utendaji chungu nzima. 

Maswali kwa msomaji:

1. Ni hatua zipi ulizozichukua kukuza biashara yako?

2. Umefanya uchanagnuzi wa UUNT (Uwezo, Upungufu, Nafasi na Tishio) ya kampuni lako? Je, unajua Uwezo, Upungufu, Nafasi na Tishio kwa biashara yako?

3. Ni nini athari za biashara yako kwa jamii yako?

Lessons

1. Uvumbuzi: Usiisahau bidhaa. Sisitizia uundaji wa bidhaa bora iliyo mpya na bunifu na inayoweza kushindana sokoni. Mara kwa mara, biashara zinahimizwa kufikiria juu ya kutangaza bidhaa na vilevile elimu ya soko. Hata hivyo, bila bidhaa nzuri, biashara haitafaulu kufaulu.

2. Usimamizi: Bidhaa bora lazima itimize mahitaji yote rasmi na kutii masharti ili  iingie katika masoko mapya. Inaweza kuonekana ghali mwanzoni kuifanyia bidhaa haya lakini hatimaye uwekezaji wako utafaidika. Hakikisha kwamba bidhaa yako ina vibali ambavyo soko linahitaji.

3. Uwenza: Uwenza/uwenzi ni muhimu katika kukusaidia kupata soko lako. Nchi zingine huendeleza maonyesho ya biashara na warsha ambapo utaweza kukutana na watu ambao wanaweza kukusaidia katika harakati zako za kufika sokoni. Fanya juu chini kushiriki katika mipango hizi na kutalii nafasi za soko mpya.