Malenge huokoa maisha. Zina kaidi kiangazi na vilvile zimejaa virutubishi zinazokinga dhidi ya unyafuzi unaohofisha na inayosababishwa na uhaba wa protini. Katika nchi yangu Uganda, wanawake wengi wanapanda malenge machache mwaka mzima ili kuyadumisha afya bora ya familia zao. Wanauza malenge yanayozalia katika soko la mitaani.
Miaka mingi iliyopita, nilianza kuwasaidia wanawake kuyaongezea thamani mmea wao wa malenge ili kuboresha maisha yao. Niligundua kwamba mahitaji yao yalikuwa rahisi kiasi: mbegu nzuri na mbinu na nyenzo mwafaka za ukulima, mbinu kiasi za kutafuta soko na zile kifedha; na kisha, kupata mkopo kiasi. Lakini, ya muhimu zaidi, nilifikiria kwamba walihitaji ujasiri. Walihitaji kujipanga na kufanya kazi kwa vikundi. Halafu wangekoma kufikiria kwamba mtu mwenye elimu rasmi chungu nzima pekee ndiye anaweza kuendesha biashara yenye fanaka.
Katika mwaka wa 2012, nilianza kwa kuwaleta pamoja wanawake wa mitaani kutoka wilaya za Mityana na Mubende zilizoko Uganda. Azimio langu zilikuwa rahisi kama mahitaji yao: kuwasaidia kuimarisha mapato ya familia zao na kuwapa uwepo wa kudumu wa vyakula: kuwasaidia watoto wao na jamii zao kukwepa utapiamlo; kupunguza ukosefu wa kazi miongoni mwa wanawake; na kukomesha uharibifu wa mashamba kwa kuwafundisha wakulima wanawake mbinu za kuwajibika.
Nilianzisha Josmark International (U) Ltd, inayojulikana miongoni mwa wakulima wanawake kama “ Biashara ya Kuongezea Malenge Thamani”. Kwa sasa, ina wafanyikazi wa kudumu watano wakiwemo wanawake watatu na wanaume wawili.
Kupitia usaidizi wa kampuni langu, wakulima wanawake wanatengeneza na kuuza bidhaa za malenge kama vile juisi, mvinyo, unga yenye rangi ya kijani kibichi unaotengenezwa na matawi na maua, mbegu zilizobanikwa, na unga wa malenge unaotumiwa kutengeneza mkate, keki, biskuti, bajia, na mchuzi. Hakuna chochote kinachotupwa- nyama ya malenge na maganda yake yanatumiwa kama chakula cha wanyama na mbolea.
Nilianza kwa kiwango kidogo nikitengeneza bidhaa za malenge pekee yangu kulijaribu soko. Bidhaa zangu za malenge zilizoongezewa thamani zilikuwa mbegu na unga wa malenge. Bidhaa hizo zilihitaji uwekezaji wa rasilmali wa kiasi kidogo na nilijua zilikuwa na faida zaidi za kiafya za lishe.
Mwanzoni, nilisaga unga huo kwa kutumia mota nilizonunua huku nyumbani na kuzirekebisha. Baadaye, niliweza kununua mashine ya kusaga iliyotengenzwa humu nchini kwa kutumia faida zangu.
Nilipata ushauri kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Leba kuhusu jinsi ya kupanua biashara yenyewe. Nilipata usaidizi wa kifedha kutoka kwa SEED Initiative ambayo pia ilinisaidia kutengeneza mpango wa biashara na kupitia utafutaji wa soko, kufunga katika furushi, na kutengeneza bia.
Kwa sasa, kampuni langu liko na biashara tano mbalimbali zinazowapa kazi wanawake hamsini wanaokuza malenge na kuziongezea thamani mazao yao.
Wateja wa kampuni hili ni hosipitali, shule, mikahawa, hoteli, na watu wanaotaka kuwapa watoto wao vyakula na vinywaji vyenye virutubishi. Tanuri mikate za kibiashara hununua unga wa malenge wa kuokea mkate, keki, biskuti, na mbegu zilizobanikwa za kampuni zina soko kubwa sana kama snacks yenye afya bora. Vilevile, tunasupply kwa HIV organizations kote nchini Uganda.
Nimetumia mbinu zote za kutafuta soko ambazo ningeweza kufikiria, nikienda sehemu mbalimbali kuwafunza watu kuhusu faida za kiafya za malenge na kutumia mitandao ya makundi ya kujiweza ya wanawake, maonyesho ya kando ya barabara, brosha na mabango na kupitia mlango kwa mlango. Soko la biashara ya malenge inakua kwa sababu inaleta faida za kijamii, kimazingira, kiafya na kiuchumi.
Maswali kwa msomaji:
1. Je, unazitumia kikamilifu malighafi zote zinazotumika katika biashara yako? Je, malighafi zingine zawezatumika kutengeneza bidhaa zingine?
2. Je, umewauliza wateja wako, mwenzako katika biashara, na watu wanaofahamu biashara yako wanachofikiria kuhusu bidhaa au huduma zako?
- Ustawi wa bidhaa: Vumbua na utengeneze thamani kwa kuongeza hadi kwa upeo matumizi ya malighafi zako.
- Uchanganuzi wa soko: Ijaribu bidhaa zako mpya kabla ya kuzitengenezwa kwa kiwango kikubwa, yaangazie ushindani yakini na uhakikishe kuna soko kwa bidhaa zako.
- Upanuzi wa soko: Watambue wateja wapya na ufikirie kuhusu njia za kutengeneza masoko mapya kwa bidhaa zako.