Kuaminika na kujiamini, wafanyikazi, na wenzio ni muhimu kwa mafanikio ya biashara yako.

Submitted by admin on Fri, 02/13/2015 - 00:00
Display title
Kuaminika na kujiamini, wafanyikazi, na wenzio ni muhimu kwa mafanikio ya biashara yako.
Bio
Image
Display name
Bilha Maina – Kenya
Bilha Maina Soko na Usimamizi wa Mikakati. Amefanya kazi katika mashirika ya kibinafsi na yale ya serikali na kwa sasa ni mjasiriamali wa kijamii. Bilha ni Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Promotions and Marketing Company (H) Ltd – KPMC. Amechangia utengenezaji wa mahtaji ya bidhaa na huduma mbalimbali za Kenya katika soko la kimataifa. Yeye pia ni mshauri wa Uendeleshaji wa Biashara na vilevile mkufunzi anayeamini kuwa uwezo mkubwa wa ushamiri wa ghafla na ukuaji wa uchumi wa Kenya upo katika uimarishaji wa ukuaji wa biashara ndogondogo na zile za kati. Bilha ana imani katika Ushirikiano baina ya mshirika ya Umma na yale ya Kibinafsi na anataka kuzisaidia jamii na serikali kufanya kazi pamoja katika miradi inayoendeleza utengenezaji wa mali. Anazisaidia biashara kushirikiana na serikali kupitia utetezi wa sera zilizofanyiwa utafiti kabambe.


Story

Mojawapo ya shida kuu ambayo wanawake wa Kenya hukumbana nayo ni jinsi ya kuweka nafaka wanazokuza. Kwa kawaida, huwa wanaziuza ili kulipa karo na gharama za matibabu. Lakini, wanaweka magunia mawili au matatu ya kulisha familia zao hadi mavuno yajayo. Wanawake wengi wanasema kwamba wanao wasiokuwa na kazi wataziuza nafaka hizi ili kupata kichele au pesa za kununulia vitu vidogovidogo huku wakitaka kulishwa bado. 

Niligundua kwamba kampuni langu lingewasaidia wanawake hawa kwa kuwapa pahali pazuri pa kuweka nafaka zao. Tuliwahimiza wanawake kujiunga pamoja katika makundi na kuzileta nafaka zao kwa ghala letu la jamii.

Nilianzisha kampuni langu, The Kenya Promotions and Marketing Company, KPMC, katika mwaka wa 2003 kwa sababu nilikuwa na nia ya kuwatia moyo wakenya kutumia teknolojia mpya na kuwasaidia kufikisha mazao yao sokoni. Tuliweza kupata kandarasi ya kusambaza nafaka kote Afrika Mashariki kutoka kwa mzalishaji wa Hermetic storage inayojulikana kama GrainPro.

Hii ilijitokeza kufaulu sana baina ya wanawake wakulima, na kazi yetu ilizungumziwa kiasi kwamba tulipewa kandarasi na East Africa Malting Limited ya kupanda mtama nyeupe ya kutengeneza pombe. Kuna soko kubwa sana kwa hii lakini wakulima ni wachache sana waliokuwa tayari kujihusisha na kandarasi ya uzalishaji kwa sababu zinafadhiliwa vibaya sana. Benki hazitawapa wakuliwa pesa wanazohitaji bila dhamana ya mkopo.

Hivyo basi, tulifikia kuhusu kilichohitajika na tukawapa wakulima wanaotoka kaunti ya Tharaka Nithi zana za kukuzia mtama. Zana hizo zilijumuisha mbegu, madawa za kuangamiza wadudu, na bima ya mimea. Ili kupata zana hiyo, wakulima wanatoa kipande fulani cha mazao yao kama amana/rubuni. Pesa zinazosalia wanakatwa kutoka kwa faida wanazotengeneza kutokana na kukua mtama.

KPMC hujenga vituo vya kukusanyia mazao hayo, hutoa turuba za kukaushia na huduma za kupura, hutumia vitanga vya mizani vya kielektroniki ili kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri. Pia KPMC hutoa lori ya kuchukua na kupeleka mazao hayo kwa kampuni la kutengeneza kimea cha pombe yakiwa kwa hali nzuri.

>Kwa vile mzigo wa kifedha umepunguzwa, maelfu ya wakulima wadogo wanataka kushiriki. Hii inapanua kiwango cha mtama katika kampuni letu na uwezo wetu wa kutimiza mahitaji ya kampuni lile la kutengeneza pombe.

Kwa sasa tumeanza kungalia sekta zingine zikiwemo zile za maziwa na kilimo cha bustani. Tunabadilisha jinsi jamii zinazalisha bidhaa na tunataka kuwasaidia kutengeneza njia za kudumu za kufanya mambo. Hii ni muhimu sana kwa maisha ya watu. Mwanamke aliye na kandarasi ya mzalizaji ana uwezo wa kuahidi shule wanakosoma watoto wake kwamba ataweza kulipa karo kwa mfumo wa malipo ya kidogo kidogo jambo linalowawezesha watoto wake kubaki shuleni mihula yote kwa mwaka. 

KPMC ipo njiani kutimiza ndoto ya kufanya kazi na familia 40, 000 ifikapo mwaka wa 2017. Kwa usaidizi wa kudumu kutoka kwa wenzetu, bidii ya wafanyikazi wetu na Rehema zake Mungu, tutafaulu.

Kuwa mwanmke mjasiriamali imenifunza mengi na ninahisi heshima nyingi kushiriki hekima yangu na wanawake wengine wajasiriamali. Yafuatayo ni baadhi ya mafunzo muhimu niliyojifunza katika njia hii.

Maswali kwa msomaji:

  1. Umechukua hatua zipi kuwa kielelezo mzuri kwa wafanyikazi, wenzako na wateja wako?
  2. Unachukua hatua zipi kujenga na kulinda sifa nzuri za biashara yako katika jamii yako? Inaathiri vipi kudumishwa kwa shughuli na pesa za biashara yako?
Je, Wajua? 

Kuaminika ni hisia ya heshima na imani ambazo unaweza kuzipitishia wengine. Hamna njia moja ya kujenga kuaminika. Ni jumla ya tabia zako, ujuzi, uwazi, ukweli, jinsi unavyowasiliana na unavyothibiti hisia zako miongoni mwa vitu vingine. Na inachukua muda, uvumilivu na kuwa na msimamo thabiti kuijenga. Wajasiriamali na viongozi wa kibiashara wote wanahitaji kuaminika ili kukuza bashara zao. Wateja hawataki kununua kutoka kwa biashara wasioamini.

Lessons

1. Uongozi: Thibitisha uongozi na uwatie motisha wafanyikazi wako kwa kuwa mfano wa bidii. Usiogope, wanaume kwa hakika wanahitaji uongozi na mchango wetu. Wako tayari kukusikiza na kukuunga mkono. Usife moyo. Wakati mambo yanaonekana magumu sana, itakuwa hivyo kwa sababu uko karibu kutoboa. Unapohisi kana kwamba mawazo yako hayafanyi kazi, ni wakati wa kuvumbua. Angazie lengo la mwisho kila mara.

2. Uthibiti wa sifa nzuri:Kuaminikani kitu cha maana. Ili kupata biashara, lazima uaminike. Ninayamaanisha maneno yangu na ninajikakamua kufanya kazi za kiwango cha juu kila mara.

3. Kupanga: pata nafasi ya kupanga haswa mpango wa kukua. Kuwa na mpango ni sehemu muhimu sana ya kujenga imani. Kujenga biashara yako kwa kupiatia mpango mzuri hukuweka katika barabara, hukuepusha na makosa na kupoteza kuaminika na vilevile kutopoteza imani yako. Mbingu ndio limit ya biashara lakini kuwa na uvumilivu wa kutosha wa kutekeleza mipango yako ya kukua hatua moja baada ya nyingine.

4. Kusimamia rasilmali za kibinadamu: Fanya kazi nyingi zaidi; unahitaji kujifunza kila kipengele cha biashara yako. Hakuna kazi iliyo duni sana kwako. Wafanyikazi wako watakuangalia kwa makini sana na kuyafuata unayofanya. Watafute wafanyikazi waliofuzu wenye ujasiri na ndoto. Wanachangia mawazo makuu na kusaidia kuendesha biashara yako na kuifanya ikue.

5. Uthibiti wa pesa: Mapato halisi ni ya muhimu sana. Zipeleke kwa benki pesa zote zinazotoka kwa biashara; wakati mwingine, zipeleke benki pesa zako za kibinafsi wakati biashara inapopitia magumu. Ziweke akaunti nzuri na uhakikishe zimekaguliwa kwa sababu muamana ni muhimu sana. Biashara inapokua, unahitaji kutumia pesa nyingi lakini wateja wengi hawalipi kwa wakati ufaao. Benki lako litakunusuru iwapo unawezakopeshwa, uko na mapato halisi nzuri na wakati mwingine ukiwa na mali.