Wape motisha na uwafunze wafanyikazi wako na uwaandae kukusaidia kukuza biashara yako.

Submitted by admin on Fri, 02/13/2015 - 00:00
Display title
Wape motisha na uwafunze wafanyikazi wako na uwaandae kukusaidia kukuza biashara yako.
Bio
Image
Display name
Adisa Lansah Yakubu – Ghana
Adisa Lansah Yakubu ni Mratibu wa Mtandao wa Afrika 2000 tawi la Ghana. Mtandao huu umekuwa ukifanya kazi na vikundi vya wanawake katika jamii ambazo zimetengwa haswa katika eneo la Kaskazini mwa Ghana ili kuimarisha maisha yao kwa kuwapa shughuli zinazoleta mapato na elimu juu ya kijinsia na uzazi.


Story

Nimekuwa nikifanya kazi na wanawake kule vijijini Ghana kwa muda wa zaidi ya miaka 26, na ninaamini kwamba umaskini wa wanawake unaweza suluhishwa na wanawake wenyewe. Katika Ghana Kaskazini, kila mtu anafahamu jinsi ya kutengeneza siagi ya shea. Hivyo basi nilipowauliza wanawake wanaotoka maeneo ya vijijini wanipe mawazo yao kuhusu jinsi wanavyoweza kuepukana na umaskini, hii ndio bidhaa waliochipuka nayo kwa pamoja.

Shida ya kwanza ya kutumia siagi ya shea inayotengenezwa na wanawake wenyewe ni kwamba sio ya ubora wa juu. Ili kushindana vyema katika masoko ya kitaifa, ilitulazimu kuwafunza wafanyikazi wetu wanawake kutengeneza siagi ya shea na kuiweka katika vifurushi kwa njia inayopendeza. Tulikuwa na wafanyikazi nane hivyo basi tulitengeneza mafunzo ya utendaji zaidi yenye picha ili kuwawezesha  wanawake zaidi ya 700 katika shirika letu ambalo karibu hawana elimu rasmi kabisa ili kuelewa mafunzo hayo.

Niliomba usaidizi kutoka kwa Japan International Cooperation Agency. Kundi la wataalamu na idara ya utafiti kutoka Chuo kikuu cha Masomo ya Maendeleo iliyoko Tamale walitengeneza mwongozo wa mafunzo tunaotumia kwa wanawake ambao wanavuna njugu za shea na wale wanaotengeneza hizo siagi. Vilvile, tulipendekezwa kuimarisha maeneo ya kutengenezea siagi.

Kisha, hao wanawake wafanyikazi walitengeneza shirika lenye matawi katika vijiji vingi. Wanawake wengine pia walionyeshwa jinsi ya kuwafunza wanachama wapya wa PagSung (wanawake wakamilifu) wavunaji wa njugu za shea na Shirika la Watengenezaji wa siagi ya shea. Mfadhili alinilipia pamoja na wanawake wengine kuzuru Shirika la Wanawake wanaojiajiri lililoko India ambapo tulijifunza mengi kuhusu ujenzi wa biashara ya mitaani.

Mwanzoni, tuliuzia masoko ya humu nchini siagi ya shea zetu kwenye kapu zilizokuwa wazi lakini tulihitaji vifurushi vizuri zaidi ili kuuza siagi zetu ng’ambo. Tulijaribu njia mbalimbali kabla tuamue kuzifunga siagi zetu kwa masanduku mangavu ya kilo 20. Siagi ya shea ya kwanza tuliyoitengeneza na iliyoimarishwa haikupokea matokeo mazuri tu bali pia ziliuzwa kwa bei za juu. Hiyo siku ndiyo ilikuwa siku ya “kwa hivyo, tunawezafaulu”

Sasa tunatengeneza pia sabuni kutokana na siagi ya shea ambazo zinaleta hata pesa zaidi. Tunatengeneza aina mbalimbali za sabuni zikiwemo baobab, moringa, hena, neem (wanawake wwenine wazee hutngeneza mafuta ya neem) na hata sabuni nyeusi ya potashi.

Wengi wa wanawake hawa waligundua kuwa kutosoma kwao kuliwafanyia kupima vitu sawasawa kuwa ngumu. Hivyo basi tuliweka alama kwa mikebe. Lakini pia tumeanzisha madarasa ya kujua kuandika na kusoma. Kwa sasa hivi, tunahitaji ufadhili mwafaka wa kifedha utakaotuwezesha kupata vifaa vya kusoma na kuwalipa walimu. Iwapo wanawake watajifunza kusoma na kuandika katika lugha zao zenyewe, wataweza kuandika tajriba zao tamu. Kuelimika pia kutawasaidia mbinu rahisi za uwekaji hesabu. Wanawake hawa wako na mengi ya kushiriki kuhusu maisha haswa juu ja jinsi ya kukabiliana na wasiwasi wakati magumu.

Mwanzoni, kila kundi la jamii lilifunzwa kutumia Susu – yaani mfumo wa akiba kwa watu maskini nchini Ghana. Kwa sasa kila kundi limefunzwa kuendesha akiba za mittani na mashirika ya mikopo. Wanawake wengine wamenunua shamba na wengine hata wamejenga nyumba za kuwakodeshea watu. Shirika letu limefaulu kiasi kwamba wanawake wengi wanajiunga nasi kila mwezi. Hii inamaanisha kwamba watakuwa wakifanya kazi ambazo wanamiliki na zinazowapa faida kikamilifu.

Wengi wa wateja wetu wanatoka Japani an Ujerumani huku wachache wakiwa wa Marekani Kaskazini. Kuwadumisha wateja wetu hakujakuwa rahisi kwani lazima tufanye bidii kuimarisha thamani na ufungaji wa wa bidhaa zetu. Pia tunapanda miti mingi ya shea ili kuidumisha biashara yetu. Hatari kubwa zinaegemea mabadiliko ya hanga yanayokwamiza ukuaji wa haraka wa miti yetu. Gharama za juu za maisha pia zinaweka shinikizo katika mapato ya watu hivyo basi zinapungua mauzo yetu. Tunatumai kwamba ununuzi wa bidhaa zetu utaimarika tena hivi karibuni.

Maswali kwa msomaji:

1. Je, waweza kupata rasilmali kutoka kwa jamii yako ili kusaidia kugundua a wazo nzuri la kibiashara, au kupanua na kukuza biashara yako?
2. Ni vipi wafanyikazi au wagavi wako wanaweza kunufaika kutokana na kujipanga na kutumia mbinu ya ujima kupata uungaji mkono, mafunzo, na ushauri?

3. Je, watambua na kutuza mafanikio ya wafanyikazi wako, wenzi wako wa kibiashara  na watu wanaosimama na bashara yako?

4. Unawasaidia vipi wafanyikazi wako kutambua vizuri talanta na uwezo wao?
5. Je, umetambua njia za uvumbuzi za kuwasaidia wafanikazi wako kuweka thamani katika maisha yao kibinafsi na jamii zao?

Lessons

1. Kuwafunza na kuwaendeleza wafanyikazi kila mara: Ndoto ya muda mrefu ya kukuza ujuzi na talanta za wafanyikazi wako isaidia kudumisha ukuaji wa biashara yako.

2. Kusimamia rasilmali za kibinadamu: Hakikisha kwamba wafanyikazi wako wana hekima, ujuzi, na mafunzo zinazohitajika kukuza biashara yako na kuwaruhusu kufanya kazi vizuri.