Tenganisha pesa za kibinafsi na zile za biashara ili kuisaidia biashara yako kukua.

Submitted by admin on Fri, 02/13/2015 - 00:00
Display title
Tenganisha pesa za kibinafsi na zile za biashara ili kuisaidia biashara yako kukua.
Bio
Image
Display name
Olivia Ogbuaku – Nigeria
Olivia Ogbuaku ni Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Olivia’s Juices nchini Nigeria.


Story

Kampuni yangu, Olivia Juices, hutengeneza maji ya matunda kwa asilimia moja ya matunda halisi. Ili kulifanya kampuni hili faulifu, ilinibidi kupitia mafunzo ili kuthibiti pesa za kampuni langu.

Naipenda sana ninachofanya lakini kulikuwa na mambo mengi ambayo sikuyajua, haswa kuhusu menejimenti ya fedha. Sikuwa na uwekaji hesabu wowote. Sikuwa nikiweka rekodi zozote za pesa. Nilikuwa nikiandika mauzo yangu ya kila siku na pia nilikuwa nikiandika vyote nilivyonunua sokoni. Hayo tu ndiyo mambo mawili niliyoyafanya.

Nilikuwa na akaunti ya benki, lakini labda kwa mwezi mzima, skutembelea benki. Nilikuwa nikitumia pesa kutoka kwa mauzo yangu kwa matumizi yangu ya kibinafsi na yale ya familia yangu. Hakukuwa na tofauti baina ya akaunti yangu ya kibinafsi na ile ya kibiashara. Kila kitu kilikuwa kimevurugwa tu.

Sikujua jinsi ya kuwaongoza wafanyikazi wangu. Hata ingwa nilikuwa tu na mtu mmoja. Sikujua jinsi ya kumwongoza.

Baada ya kupokea mafunzo, nilikuja kuwa msisitizi zaidi. Kwa sasa uwekaji hesabu yangu ni sawasawa kabisa. Tunaweka pesa za kila siku kwa benki kila jioni kabla benki kufungwa, bila kujali kiasi cha pesa hizo. Nimetenganisha biashara na akaunti yangu ya kibinafsi. Nikikopa kutoka kwa biashara yangu, lazima nilipe. Vilevile  iwapo biashara imenikopa lazima inilipe ifikapo mwisho wa mwezi. Isitoshe, nimeweza kujilipa mshahara.

Nimetengeneza aina ya bidhaa yangu na nimeweka vitambulisho venye maelezo katika masanduku zangu ziitwazo Olivi’s Juice. Nina watu nwawili katika uzalishaji na mkurugenzi mmoja wa kutafuta soko ambaye huenda nje kutafutia hafla. Ninapanga kuwaajiri watu wengine zaidi mwaka huu.

Kwa sasa nina kibanda. Nawafikia wateja wangu kupitia ujumbe mfupi kwa simu ya mkono. Huwa wanakuja na vilevile kuwaelekeza wengine kwangu. 

Maswali kwa msomaji:

1. Je, unaweka rekodi ya shughuli zote za biashara yako?

2. Je, unatenganisha peza zako za kibinafsi na pesa ambazo biashara yako imekutengenezea?

3. Je, una mshauri wa benki anayeweza kukueleza jinsi ya kuendesha akaunti ya benki?

Lessons

1. Uwekaji hesabu: Ili kuendesha biashara yako kwa ufanisi, fuatilia kuingia na kutoka kwa pesa zako (mapato na matumizi yote). Uwekaji hesabu makini inahitajika ili kufuatilia ukuaji wa biashara yako na kujua mauzo yako yanapodidimia.

2. Kufanya uamuzi: kuweka rekodi sawa ya pesa hukuwezesha kufanya uamuzi juu ya matumizi ya fedha za biashara kama vile kujilipa mshahara mara kwa mara, kuwaajiri wafanyikazi, kununua vifaa, na kulipia utafutaji soko na uhamazishaji wa bidhaa.

3. Kuweka pesa kwa benki: Benki itakuwa tayari kukupa deni na mikopo ukiwa na rekodi ambazo ziko sawa. Hii itakusaidia kuwanasa wawekezaji.