Rebecca ni mkulima kutoka wilaya ya Mpigi kule Uganda. Wilaya hii imejitenga. Alipopata paneli ya jua kuangazia, alikuwa anataka kuiweka katika nyumba ya kuku. Alijua kwamba kuku hula tu wanapokuwa na uwezo wa kuona na iwapo angeongeza mwangaza, kuku wake wangekula zaidi na kuwa na afya bora. Kwa kweli, walifanya hivyo na kutaga mayai zaidi, wakazidisha mapato yake yaliyomwezesha kununua mbegu na hatimaye alinunua mbuzi, nguruwe na hata ng’ombe.
Wakati nilipokutana na Rebecca, nilikuwa na uzoefu wa miaka 20 kama mbia mwekezaji wa benki anayegemea kwa fedha za nishati na nilijua mengi kuhusu umaskini mkubwa wa nishati barani Afrika. Nia yangu ilikuwa kuwasaidia wanawake kama Rebecca kuboresha maisha yao.
Rebecca alithibitisha uwezo wa kipekee walio nao wanawake wa Afrika. Kutokana na maendeleo ya mwangaza mmoja, alitengeneza shamba lenye faida na kuimarisha hadhi ya maisha ya familia yake mwenyewe. Alijenga hata shule ambako aliwafunza watoto wenyeji jinsi ya kusoma na kuandika na vilevile namna ya kufanya kilimo katika vipande vyao vya shamba.
Ili kuwapa motisha wanawake wengi kama vile Rebecca na kuwasaidia kuboresha maisha yao, nilianzisha Solar Sister katika mwaka wa 2009. Solar Sister ni biashara ya kijamii inayotumia mfumo wa biashara unaoegemea uvumbuzi kuleta energy ya kudumu na yenye bei nafuu kwa mamilioni ya waafrika wanaoishi bila hata glopu moja.
Wanawake katika mtandao wa Solar Sister wanajenga biashara za kudumu kwa kuuza taa za jua, vifaa vya kuchaji simu za mkono, na stovu isiyoharibu mafuta. Wanazigeuza mitandao yao ya familia, marafiki, na majirani kuwa mikanda ya kufaa ya kusambaza bidhaa kijijini na wateja ambao ni vigumu kuwafikia. Katika Solar Sister, tunawafunza wafanyikazi wetu na wajasiriamali wanawake kwa kushiriki desturi nzuri, tunaweza kujenga hisia ya udada na kuimarika kila siku.
Solar Sister hivi sasa ina wajasiriamali 724 nchini Nigeria, Tanzania na Uganda na wamewapelekea zaidi ya watu 115,000 nishati safi.
Wanawake lazima wawe sehemu ya suluhisho kwa umaskini wa nishati kwa sababu 70% wa maskini wa nishati ni wanawake na wasichana. Wanawake sita kati ya wanawake waafrika kumi wanaishi katika maeneo ambapo kuni ni nadra. Wanawake wengi hutegemea kandili, ambazo ni za gharama za juu na ni hatari sana, kupata mwangaza na kupikia. Wanachomeka na vilevile wanavuta moshi za mafuta taa iliyo sawa na kuvuta sigara paketi mbili za sigara kila siku. Hii inaeleza kwa kiasi fulani kwa nini thuluthi mbili ya wanawake wanaougua kansa ya mapafu katika mataifa yanayoendelea sio wavutaji sigara.
Bila mwangaza kwa jamii, wanawake wako katika hatari za vurugu vya kijinsia wanapotembea kutekeleza shughuli zao usiku. Utunzaji wa afya ya mama huathirika panapokosekana nguvu za umeme-hebu fikiria ugumu wa kuzalisha mtoto gizani. Hii ndio sababu niliwalenga kimaksudi wanawake wanaokabiliana na umaskini wa nishati kupitia biashara yangu.
Solar Sister Iniobong Okon kutoka nchini Nigeria ni nesi mstaafu ambaye amejenga kliniki ya akina mama iliyo na stovu unatumia nishati kidogo ya kuwachemshia maji wateja wake na vilevile chumba kilichoangazwa barabara na paneli za jua. Hivi majuzi, alizalisha mwanawe mwanamke anayeitwa Blessing, ambaye mwenyewe baadaye alikuja kuwa Solar Sister kwa vile alifurahishwa sana na aliyoyapitia katika kliniki hiyo.
Mswali kwa msomaji:
- Je, umewahifikiria jinsi mahitaji ya kawaida na shida katika maisha yako ya kila siku zinaweza kuvutia suluhisho kwa jamii yako?
- Je, mfumo wa biashara yako inafaa kuhusisha mitandao ya wanawake wajasiriamali wengine kupanua usambazaji wa bidhaa au huduma zako?
1. Mikondo ya kuzambaza bidhaa: Tafuta mbinu za kushirikiana na watu, makundi ya wanawake, mashirika, makampuni na mitandao mengine yanayoweza kukusaidia na uzambazaji wa bidhaa au huduma zako kwa maeneo ambayo ni vigumu kuyafikia.
2. Uthibiti wa wafanyikazi: Shiriki ujuzi na ndoto zako na wafanyikazi wako na wenzako wa kibiashara wako kupitia mafunzo na ushauri. Unavyoendelea kufanya hivyo ndivyo unavyopata wanunuzi wengi katika biashara yako na ndivyo wengine wengi wangependa kuchangia ufanizi wake.