Mimi ni mwanamke. Mimi ni mtaalamu wa biashara. Mimi ni mjasiamali wa kijamii. Kampuni langu, The Business of Me, lilianza kama shirika lisilotengeneza faida ili kukabiliana na shida ya kitaifa ya vita vya nyumbani.
Nilikuwa nimezoea kuishi maisha mawili.Nilikuwa mkurugenzi aliyefaulu wa Wall Street lakini nilikuwa pia mwanamke aliyedhulumiwa na bwanake nyumbani. Nilipokuwa huru hatimaye, niliamua kuanzisha The Business of Me kuwasaidia manusura wengine wa vita vya nyumabi kujifunza kuzishinda hofu zao na kuishi maisha ya kujitegemea yasiyokuwa na dhuluma
Nilipoanzisha kampuni langu mwanzoni, kampuni langu lilikumbwa na hali ya hatari ya pesa. Ilinilazimisha kutafuta njia ya kulifanya kampuni langu liwe na pesa za kutosha ili kutoa huduma ambazo wanawake wengi walikuwa wanahitaji. Baada ya kufkiria sana, niliamua kutoa huduma za kampuni langu kwa makampuni kubwakubwa. Biashara ya kijamii huenda isipate nafasi katika malengo au misheni za kila shirika lakini kwangu iliwezekana.
Huduma zangu haziimarishi tu maisha ya wafanyikazi katika mashirika bali pia huimarisha eneo la kazi kwa kila shirika linalozitumia. Kwa sasa tunatoa mipango za webinar-based kwa waathiriwa na manusura katika makampuni hizi ili kuwasaidia kuishi maisha yanayojitosheleza na iliyo mbali na dhuluma za kimwili, kihisia na zile za kiuchumi huku zikiwapa motisha ya kuwa wenye faida zaidi katika maisha yao ya kibinafsi na yale ya kitaaluma. Tunatumia mbinu na masomo ya biashara na nguvu za soko ili kuendeeleza ajenda yetu ya haki za kijamii, kimazingira na kiutu.
Kama mjasiamali wa kijamii, ninaweza kutalii, kutengeneza, kutekeleza na kupanua huduma za The Business of Me kuwiana na landscape ya teknolojia inayobadilika haraka sana. Tunatumia mbinu mpya kabisa, baada ya utafiti, kuwasaidia waathiriwa kuimarisha maisha yao. Kama mmoja miongoni mwa wajasiriamali wengi, ninaamini kwamba tuko katika harakati za mbinu mpya ya kufikiria jinsi tunavyoona, kuanzisha na kuendesha biashara za kijamii.
Maswali kwa msomaji:
1. Je, ulijua kwamba wajasiriamali wa kijamii ni watu wanaojenga biashara kwa suluhisho za kubuni ili kutatua shida za kijamii zinazotatiza zaidi? Je, unayo wazo la kibiashara linaloweza kusuluhisha shida ya kijamii huku likikutengenezea pesa kama mjasiamali?
2. Je, umekuwa ukifikiria kwa makini kuhakikisha kuwa kampuni lako linawahudumia kundi kubwa zaidi la wateja kadri iwezekanavyo? Kwa mfano, kuna washika dau wengine au intermediary wanaoweza kulipia bidhaa zako au huduma kando na mtumizi/mteja wa mwisho?
1. Mfumo wa biashara: Biashara ya kijamii model inawezakukusaidia kupata faida nab ado uifanye kazi za kijamii katika jamii yako.
2. Kuzalisha mapato: Tambua njia za kibunifu za kutengeneza soko la bidhaa zako au huduma zako. Uwe tayari kuangazia pembe mabalimbali za kuipa biashara yako soko.