Kujenga biashara imara.

Submitted by admin on
Display title
Kujenga biashara imara.
Bio
Image
Display name
Anne Shongwe - South Africa
Ann ndiye Mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa Afroes Transformational Multi-Media & Consulting. Afroes ni biashara ya kijamii inayotoa na kuendeleza masuluhisho ya kiubunifu yanayotokana na turathi maridhawa ya Afrika na ambayo hujikita kwenye mazungumzo ya kutumia teknolojia shirikishi ya dijitali na habari. Dhamira ya msingi ya Afroes ni kuhamasisha mazungumzo na vitendo vya Waafrika kwa njia ya kidijitali au mazungumzo ya ana kwa ana kuhusu matumaini na uwezekano. Kwa kushirikiana na kampeni inayoongozwa na Mfuko wa Watoto wa Nelson Mandela (Nelson Mandela Children’s’ Fund) ya Kushabikia Watoto, Afroes inajenga michezo mbadala ya kidijitali ili kushirikisha na kuhamasisha utendaji miongoni mwa vijana nchini Afrika Kusini na kwenye ukanda mzima, kuhusu hatari wanazoweza kukumbana nazo wakati wa michuano ijayo ya Kombe la Dunia. Afroes imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Wakfu wa W.K. Kellogg, Taasisi ya Mstakabali wa Kiafrika (African Futures Institute), Mfuko wa Watoto wa Nelson Mandela na Akademia ya Uongozi wa Kiafrika (African Leadership Academy).

please enter text for building a resilient business

Story

Dhamira ya Afroes ni kutumia teknolojia ya rununu kutalii uvumbuzi katika kusoma. Huku asilimia 70 ya vijana wa Afrika tayari wakiwa na rununu, ndoto yetu ni kupata njia za haraka na za kiubunifu za kuwapa ujuzi wanaohitaji kufikia nafasi mbalimbali. Kufikia sasa, Afroes imeunda masuluhisho ya masomo kutumia michezo ya rununu ambayo imefikia watumiaji zaidi ya 500,000 ambao wamekabiliana na masuala yenye utata ya stadi za maisha. Haya ni pamoja na kuzuia dhuluma za kijinsia na kuwatambulisha katika ulimwengu wa kazi za kibinafsi za mtandaoni. Afroes inapatikana Kenya na Afrika Kusini na imekuwa ikifanya kazi kutokea Januari mwaka wa 2010. Biashara yetu kwa sasa ina kikosi cha watu 11 katika afisi zilizopo katika mataifa hayo mawili, wakiwa ni wanawake sita na wanaume watano.

Sikukuwa na kusudio la kuwa mjasiriamali wa teknolojia. Nilitaka tu kutatua tatizo ambalo lilikuwa likinisumbua sana akilini. Kama mama wa watoto watatu warembo, nilijua kuwa kizazi cha jamii changa kilikuwa kinatekwa nyara na ndoto za michezo yao. Nilishangaa ni kwa jinsi gani watoto hawa wangepewa ujuzi wanaohitaji ili waweze kuishi maisha yenye matunda mema, kisha kulipa bara letu tukufu la Afrika uongozi wa kesho ambao bara hili litahitaji.  

Baada ya majaribio mengine ambayo hayakufanikiwa ya kumshawishi mtoto wangu mvulana dhidi ya kutumia muda mwingi kwenye kifaa chake cha kuchezea michezo ya video cha Xbox, nilipata utambuzi mkubwa. Niligundua kuwa kama tungeibuni michezo ambayo ingeyateka nyara mawazo ya watoto kama yeye, lakini iwe michezo yenye maudhui na mafundisho ambayo yanazielekeza fikra zao kuwa na maadili, ujuzi na maarifa ambayo yatawaandaa kwa maisha mema na uongozi bora, hilo lingekuwa jambo zuri sana.

Lakini ilikuwa changamoto kuu. Sikuwa na maarifa ya kiufundi, na kupita kizuizi hiki, kulinitia wasiwasi sana hadi kwa miaka kumi kabla sijaanzisha Kampuni ya Afroes, nilishinda nikijaribu kadri ya uwezo wangu kuondoa wazo hilo. Sikufua dafu. Kwa hivyo, miaka minne iliyopita, wakati muda ulipowadia, niliacha kazi ambayo ilikuwa rahisi na ya kupendeza yenye mapato mazuri niliyokuwa nikifanya katika Umoja wa Mataifa kisha nikaanza safari ya giza ili kuweza kutimiza maono yangu.

Nilitaka kuunda michezo ambayo ingeweza kubadili fikra za mamilioni ya vijana wa Kiafrika, kuwasaidia kuwa watatuzi wazuri wa changamoto za maisha, wanaongozwa na maadili ya usawa na wenye maono halisi ya mafanikio kwao wenyewe na kwa Afrika.  

Je, niliwezaje kufanya jambo hili ambalo lilioneka kuwa gumu kwa muda mrefu? Naam, kwa kuanza, nilitafuta watu werevu ambao wangenisaidia. Nilipata watu katika mtandao wangu na katika jamii ya Michezo kwa Mabadiliko (Games for Change Community) ambao walikuwa radhi kunipa ushauri wa hekima na maarifa. Kundi la wasomi wa Uzamili katika Biashara kutoka Oxford, Uingereza, wakiongozwa na rafiki yangu mdogo kutoka Kenya walinisaidia katika kufanya utafiti wa hali ya soko na mpango wa biashara.

Kufupisha kisa changu, sasa hivi tuna kikosi cha wanawake sita na wanaume watano ambao wako Kenya na Afrika Kusini, wote wakiwa vijana werevu sana ambao wanaelewa mahitaji ya kibiashara na kiufundi ya Afroes. Tayari tuna mafanikio mawili makuu – mchezo wa kupinga dhuluma kwa watoto ili kulinda watoto wakati wa Kombe la Dunia la mwaka wa 2010 huko Afrika Kusini, na MORABA, mchezo ambao unawafundisha vijana kukabiliana na dhuluma za kijinsia. Mchezo huu tayari una watumiaji zaidi ya 100,000 katika Afrika Kusini na una uwezekano wa kutumika shuleni mwaka huu (2015). 

Dhamira ya Afroes ni kutumia vizuri teknolojia ya rununu katika masomo na tayari tunakaribia kufikia watumiaji 500,000. Zaidi ya asilimia 70 ya vijana wa Kiafrika wana rununu na ndoto yetu ni kupata njia za kiubunifu na za haraka za kuwafundisha ujuzi wanaohitaji ili kuwa na mafanikio, njia hizo zikijumuisha kubadili mielekeo yao pamoja na mikakati mingine kama vile kuwaingiza kwenye ulimwengu wa kujifanyia kazi kwenye mtandao.

Katika kila hatua tunayopiga, wanawake wamekuwa nguzo kuu katika kukua kwetu. Wanawake ambao wanaongoza biashara na wanawake ambao wanaendesha miradi mbalimbali wamejitolea kuhakikisha kwamba tunapata kandarasi, wamejaribu huduma zetu, na kuhakikisha wamepata mikataba.

Kwangu na kwa wale ambao wameungana nami, Afroes imekuwa safari nzuri ajabu ya kujifunza mengi, kukua na ya mwamko mpya. Tuna maono makuu kwamba tutasonga mbele na ingawa wakati mwingine utakuwa mgumu sana, biashara ya wanawake inahitaji kujitolea na ustahimilivu; mtandao ule dhabiti wa wanawake wengine ambao tutajenga biashara yetu kwao na kupitia wao. Kila mwanamke anastahili kujaribu angalau mara moja katika maisha yake. Inabadili maisha! 

Lessons

1. Kila mjasiriamali anaongozwa kila siku na lile tatizo na dhamira ya awali inayomsukuma. Liandike kisha ulitundike mahali ili kila mtu alione. Wakati biashra yako inapitia changamoto nyingi – kama itakavyopitia kwa hakika – unahitaji kukumbuka ni kwa nini ulianza safari hiyo ili kwamba uweze kugundua upya motisha wa kukuwezesha kuendelea.

2. Tafuta wanaume na wanawake ambao ni werevu zaidi yako katika maeneo muhimu ya biashara yako ili wakusaidia kutekeleza maono yako. Biashara nyingi zinapitia changamoto kwa sababu wamiliki wanaogopa kutafuta wosia kutoka kwa watu wenye maarifa zaidi yao.

3. Anza na watu unaoweza kuwashawishi kwa urahisi – watu ambao wanakujua na wanakuamini na wanaamini kazi yako – kisha wekeza katika kuimishara ushawishi huo. Tafuta wanawake kutoka kwenye kampuni za wateja ambao wako radhi kusikiliza sababu zako za kuyafanya yale uyafanyayo na uwashawishi kuwekeza katika mradi – hata kama hatua hii inaonekana yenye  hatari za aina fulani.