Kadiria nguvu, upungufu, nafasi na yakini ishara za atari kwa biashara yako.

Submitted by admin on Fri, 02/13/2015 - 00:00
Display title
Kadiria nguvu, upungufu, nafasi na yakini ishara za atari kwa biashara yako.
Bio
Image
Display name
Chunhong Chen - China
Chunhong Chen ni mtaalamu wa kutoa suluhisho kwa mtumiaji wa mwisho wa mbinu za kuokoa maji. Anamiliki vibali rasmi vingi vya kuzalisha teknolojia ya kuokoa maji nchini Uchina. Ubingwa na mapendeleo yake yako katika hatua anuwai za maisha ya bidhaa na mifumo ya uvumbuzi wa biashara.


Story

Kujenga biashara haikuwa azma yangu ya mwanzo. Nilikuwa nataka tu kumsaidia babangu kuitumia teknolojia yake ya maji. Lakini ilikuwa funzo gumu kijifundisha. Iliyonisetiri katika wakati wangu mgumu zaidi ilikuwa ni imani yangu kwamba hoja la kuweka akiba pamoja na teknolojia ya babangu zingeweza kutangazwa kote ulimwenguni ili dunia yetu iwe imeimarika.

Nilikulia eneo moja kule Uchina mashambani. Hata hivyo, nililazimika kuacha shule na kumsaidia babangu kwa kuchukua majuumu magumu ya kiwanda. Baadaye, nilijifunza Kiingreza na Somo la Fedha na hatimaye nilifuzu kama mwalimu. Mnamo mwaka wa 2007, niliacha kazi yangu ya ualimu, nikauza nyumba yangu na kung’oa nanga kuelekea jiji la Shanghai kueneza teknolojia ya babangu ya choo kinachotumia maji machache. Ilikuwa hatua ya kijasiri. Ingawa bwanangu aliuunga mkono uamuzi wangu, babangu aliyebuni technolojia hiyo alikasirika kwamba niliacha kufunza. Kule Shanghai, nilipambana mwanzoni kwa kukosa rasilmali, mahusiano na ufadhili- yote hayo hayaepukiki katika kuanzisha biashara katika mazingira mapya na yenye ushindani. Bila pesa za kuhamasisha nilichukua kazi ya kutangaza bidhaa yangu pekee yangu: niliongea na watu katika mabasi na kuonyesha bidhaa zangu kando ya barabara; popote pale ningevuta nadhari ya watu. Bila pesa za kuajiri wafanyikazi, nilipeleka vyoo na kuziweka pekee yangu. Nilikumbana na vizingiti chungu nzima zikiwemo upungufu wa tajriba ya biashara, rasilmali ndogo ya kuanza na kutojihusisha na kushuku kwingi. 

Katika mwaka wa 2009, nilipata pumziko nilipogundua bustani la viwanda ya kuokoa nishati na biashara za utunzaji wa kimazingira katika wilaya ya Honkou jijini na kuihamisha biashara yangu hadi kwa jengo liliokuwa likiendelea kujengwa. Hata hivyo, kwa vile singeweza kumudu kodi ya nyumba hiyo, nililazimika kuwashawishi waendeshaji wa bustani hiyo ya viwanda hiyo kuniruhusu kuziweka vyoo zangu katika nyumba zao kwa kodi ya bure kwa miezi 6. Huu mkataba uliiandalia biashara yangu uthabiti na hatimaye ukuaji.

Katika mwaka wa 2011, nilikuwa mchina wa kwanza kushinda The Cartier Women’s Initiative Award ya eneo la Asia-Pacific. Kabla ya tuzo hilo watu wangeidharau kampuni langu dogo, kituo tu katika arthi kubwa sana ya China. Baadaye, walionyesha heshima nyingi sana. Tuzo hiyo lilinitia moyo wa kuifikiria tena biashara yangu na kuipanua katika bidhaa zinazotumia maji machache zingine. Singeweza faulu bila kufunzwa, iliyokuwa sehemu ya tuzo hilo. Kushiriki katika tuzo ni nafasi ya kipekee katika maisha ya binadamu ambayo kila mtu anafaa kuijaribu.

Huku jukumu la wanawake katika uwanja wa uchumi uanapoimarika, mvuto wa mwanamke katika ujasiariamali hauwezi ukaepukika tena. Ninaamini kwamba jamii yetu inafaa kuwajengea wanawake wajasiriamali mazingira mazuri. Ili kufanikisha hili, mzigo wa wanawake katika familia lazima upunguzwe. Wanaume wanafaa kuhimizwa kushiriki katika majukumu ya nyumbani kama vile kuwatunza wakongwe, watoto na kufanya kazi za nyumbani. Hivyo basi, wanawapa wanawake muda zaidi na nafasi ya kutumia talanta zao. Vilevile, pesa zaidi za wanawake wajasiriamali zinafaa kutengwa ili kuwapa usaidizi wa kifedha wa moja kwa moja. Hatimaye sera zinazopendelea ujasiriamali wa kike zinafaa kutekelezwa. Tunafaa kuzijenga taasisi za mafunzo na vitovu vya shughuli za wajasiriamali wanawake ili kushiriki maarifa na tajriba zao. Mwisho, serikali na mashirika kama vile Umoja wa Kimataifa, zinafaa kufanya kazi pamoja na vyombo vya habari kujenga a anga ambayo kijumla huwatia motisha wanawake wajasiriamali.

Maswali kwa msomaji:

  1. Je, umekadiria uwezo, upungufu, nafasi na yakini ishara za hatari kwa biashara yako? Je, umeweka mpango wa kuthibiti hatari hizo?
  2. Je, unatumia nafasi za mafunzo na ushauri kwa manufaa ya biashara yako? Unatuma maombi ya kushiriki katika mashindano, tuzo, mipango ya mafunzo, ruzuku na usadizi zingine? Wasiliana nasi katika empower.women@unwomen.org kwa maelezo zaidi kuhusu nafasi kama hizo.
Lessons

1. Uchambuzi wa SWOT: Uwezo, upungufu, nafasi na hatari kwa biashara yako zinafaa kufanyiwa kila bidhaa au huduma na mfanyiko tendani wa biashara yako. Uwezo unaojumuisha sifa za biashara yako ndio unakupa manufaa juu ya biashara zingine. Upungufu unajumuisha vizuizi vikilinganishwa na vitu vingine. Nafasi ni chembechembe ambazo ungezitumia kukuza biashara yako zaidi huku hatari kwa biashara ni zile ambazo zingesababisha shida kama hazingethibitiwa vizuri. 

2. Kuthibiti hatari: fikiria njia za kuthibiti the mashaka/hatari kwa bidhaa/huduma au biashara yako. Kuwa na usaidizi kila mara shida zikiibuka na uwe na mpango tayari kusimamia fanaka yako kwa njia ya rasilmali, wakati, leba na rasilmali. Kwa njia yoyote ile, lazima ujipange na uwe tayari.